Ni nani basi aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni? Akaita mtoto mmoja akamweka katikati yao, akasema, Amin, nawaambia, msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni. —MATHAYO 18:2–3
Kitu kimoja kizuri kuhusu watoto ni kwamba si wagumu wa kuelewa. Watakufanya ujue wanachohitaji wakati wote, watakukimbilia na kuanguka mikononi mwako wanaposhikwa na woga, na watakupa busu kubwa, wakati mwingine bila sababu. Inatuliza kuwasiliana na watoto, kwa sababu huwa hawajaribu kuficha hofu zao au hisia.
Ninaamini hivyo ndivyo Mungu anavyotaka tuwe tunapozungumza naye. Anapendezwa tunapomkaribia na ukawaida wa mtoto pamoja na imani. Kama tu vile watoto wanavyowaamini wazazi wao kikamilifu kama kawaida, tunaweza pia kuwa na wingi wa shauku na wasafi wa moyo tunapomwamini Mungu. Mweleze Mungu moyo wako wote, na ukumbuke: unaweza kumpa kila kitu katika maisha yako kujua kwamba anajali.
Mungu hatafuti uhusiano wenye mambo mengi. Anatafuta mioyo miaminifu na imani kama ya mtoto. Unaweza kuacha mahitaji yako yajulikane na Mungu (Wafilipi 4:6), na kumkimbilia unapohisi woga(Zaburi 91:1–7). Mungu anataka ujisikie huru kuonyesha upendo wako kwake na kumweleza yaliyo moyoni mwako kwa uwazi. Kadri unavyojifunza kuja kwa Mungu kwa imani kama ya mtoto, ndivyo utakavyokua katika uhusiano wako naye.
Hatutaki utoto katika uhusiano wetu na Mungu; tunataka kuwa kama watoto.