Omba

Omba

Msijisumbue kwa neno lolote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. —WAFILIPI 4:6

Nyakati nyingi huwa tunachukulia maombi kama jitihada ya mwisho baada ya kujaribu mengi. Sababu hutofautiana—huwa tunajaribu kutatua tatizo peke yetu, tunachukulia kwamba Mungu ana shughuli za vitu vingine vingi, au tunahisi Mungu ametukasirikia na kwa hivyo hatasikiliza maombi yetu. Lakini tunapokosa kuomba matokeo huwa yaleyale: Tunabeba mizigo ambayo hatuhitaji kubeba.

Kwa waaminio wengi, maisha ni magumu zaidi kuliko vile yanastahili kwa sababu hatutambui jinsi maombi yalivyo na nguvu Tungekuwa tunatambua hivyo, tungekuwa tukiomba kuhusu kila kitu, sio kama suluhu ya mwisho, lakini kama jambo la kwanza.

Katika Yakobo 5:13, Mtume Paulo anatoa suluhu rahisi ya maneno matatu kwa baadhi ya changamoto za maisha: “Na aombe.” Ujumbe kwetu katika msitari huu ni kwamba haijalishi kinachofanyika katika siku, tunaweza kumwendea Mungu kwa maombi. Kuna faida kubwa katika uamuzi huu—kadri unavyoomba ndivyo, ndivyo utakavyozidi kumkaribia Mungu.

Wakati wowote unapokuwa na tatizo, fanya maombi yakawe suluhu ya kwanza. Ukiwa na hitaji usisite kumwambia Mungu hitaji lako. Unapotamauka au kuhisi kukata tamaa, acha Mungu akawe mtua wa kwanza utakayezungumza naye kuhusu vile unavyohisi. Anakupenda, na unapomwendea kwa maombi, utashangaa tofauti yatakayoleta katika maisha yako.


Katika hali yoyote utakayojipata, fanya maombi yawe suluhu yako ya kwanza sio ya mwisho.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon