Ombea Wengine

Basi kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani zifanyike kwa ajili ya watu wote  (1 TIMOTHEO 2:1)

Tunapoomba, tunazungumza na Mungu na kumsikiza akizungumza nasi.  Aina moja ya maombi ni uombezi, ambayo ni kuombea tu mtu kando na wewe. Ni kumlilia Mungu kwa niaba ya mtu mwingine, kupeleka mahitaji yao kwa katika maombi, na wakati mwingine kusikia kitu kutoka kwake kuhusu hali yao. Uombezi ni mojawapo ya maombi muhimu kwa sababu watu wengi huwa hawajiombei au hawajui namna ya kuomba. Kwa nini? Kwa sababu hawana uhusiano na Mungu. Kuna nyakati pia ambapo hali zinakuwa ngumu sana, mfadhaiko uko juu, uchungu ni mwingi, au vitu vinachanganya kiasi cha watu kukosa kujua jinsi watakavyoomba kwa sababu ya hali zao. Na, kuna nyakati ambazo watu wamejiombea, wakajiombea, na kujiombea hadi wakakosa nguvu za kuomba zaidi.

Kwa mfano, nilimtembelea rafiki yangu aliyekuwa hospitali wakati mmoja akiugua saratani. Alikuwa amepigana vita vya kishujaa na kuomba kama shujaa, lakini alifika mahali ambapo hakuwa na nguvu za kutosha za kujiombea jinsi alivyotaka na akasema, “Joyce, siwezi kuomba tena.” Alihitaji marafiki wake kumwombea- sio tu kumwombea, lakini kumwombea kweli- kuomba kwa niaba yake kwa sababu asingeweza.

Nina hakika kuna watu katika maisha yako ambao wanahitaji maombi, watu wanaokuhitaji kuzungumza na Mungu na kusikia kutoka kwake kwa niaba yao. Ninakuhimiza kumwomba akuonyeshe ni akina nani na wewe uwe mwaminifu kuwaombea.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Kuwa mwaminifu kwa kuwaombea watu jinsi Mungu anavyokungoza.  

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon