Pokea Nguvu Kutoka Kwa Maombi

Naye kwa vile alivyokuwa katika dhiki, akazidi sana kuomba,hari yake ikawa kama matone ya damu yakidondoka chini (LUKA 22:44)

Wakati ulipofika wa Yesu kwenda msalabani, alivumilia mapambano makuu katika nia na hisia zake. Alihitaji nguvu za Mungu ili kutimiza mapenzi ya Mungu kama tufanyavyo wakati mwingine. Aliomba na kupokea nguvu hizo. Biblia inasema kwamba vile alivyoomba malaika walikuja na kumhudumia.

Usichukulie tu kuwa kile Mungu anachokuambia ufanye ni kigumu sana. Iwapo unahiari kufanya mapenzi ya Mungu, na umwombe Mungu kukupa nguvu, atakupa. Usiharibu maneno kumwambia Mungu na wengine jinsi kazi yako ilivyo ngumu. Tumia hizo nguvu kumwomba Mungu akupe ujasiri, udhamirifu na nguvu. Ninafikiri ni kitu kizuri kushuhudia Mungu anapoungana na mtu kumwezesha kufanya mambo yasiyowezekana.

Vitu vingi haviwezekani mtu akiwa peke yake, lakini na Mungu kila kitu kinawezekana. Pengine unakabiliwa na hatari au tatizo sasa hivi; iwapo ndiyo, ninakuomba ukumbuke mapambano ambayo Yesu alipitia bustanini. Alihisi shinikizo kiasi cha jasho kuwa damu. Kwa hakika iwapo alifanya alivyofanya kupitia kwa nguvu za Mungu, basi unaweza kupata ushindi pia kupitia kwa maombi.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Mungu hakupi kufanya chochote kinachozidi uwezo wako kufanya akiwa kando yako.   

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon