Pokea Upendo wa Mungu

Pokea Upendo wa Mungu

. . . Pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepewa sisi. —WARUMI 5:5

Biblia inatufundisha kwamba upendo wa Mungu umemiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepewa sisi. Hilo kwa urahisi linamaanisha kwamba, Bwana anapokuja, katika mtu wa Roho Mtakatifu kukaa katika mioyo yetu kwa sababu ya imani yetu ndani ya mwanawe Yesu Kristo, huleta amani naye, kwa kuwa Mungu ni upendo (1 Yohana 4:8).

Ni muhimu kuuliza tunachofanyia upendo wa Mungu ambao tumepewa bure. Tunaweza kuwa tunaukataa kwa sababu tunafikiri hatufai vya kutosha kupendwa? Je, tunaamini kwamba Mungu yuko kama watu wengine waliotukataa na kutudhuru? Ama tunapokea upendo wake kwa imani, tukiamini kwamba ni mkuu kuliko kutofaulu kwetu na udhaifu wetu?

Kwa usaidizi wa Mungu, tunaweza kujipenda—sio kwa njia ya choyo na ubinafsi inayozalisha mtindo wa maisha ya kujifurahisha, lakini kwa njia ya usawa na uungu, njia ambayo kimsingi inathibitisha maumbile ya Mungu kama mazuri na sahihi.

Huu ndio mpango wa Mungu: Ili sisi tupokee upendo wake, tujipende kwa njia ya kiungu, tumpende pia kwa ukarimu, halafu tupende watu wote wanaokuja katika maisha yetu.


Mungu anapotufikia ili atupende sisi, anajaribu kuanzisha mzunguko utakaotubariki sio tu sisi bali wengine wengi.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon