Rafiki Mzuri Sana Utakayekuwa Naye

Rafiki Mzuri Sana Utakayekuwa Naye

Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake. YOHANA 15:13

Yesu ndiye rafiki mzuri kabisa utakayewahi kuwa naye. Hata kama unahisi au hauhisi kwamba yuko hapo, yuko hapo kwa ajili yako kumtegemea katika kila eneo la maisha yako. Mwegemee na umwamini kwa moyo na nafsi yako yote. Atakupeleka upande mzuri na kunyosha njia zako. Unaweza kuongea naye kuhusu kila kitu.

Mshukuru kwa baraka ambazo amekupa—ikiwemo baraka ya uwepo wake. Huwa anakuelewa wakati wote na hakukatai wala kukuhukumu. Hakuna kilicho kikubwa kwake kushughulikia, na kwa hivyo hakuna kilicho kidogo pia. Ingawa mara nyingi huwa hatuhisi uwepo wa Mungu, tunapotia imani yetu ndani yake, tunaona matokeo yake ya kufanya kazi katika maisha yetu.


Sala ya Shukrani

Asante, Baba, kwa rafiki niliye naye ndani ya Yesu. Ninaamini kwamba huwa siwi peke yangu na nina rafiki mzuri sana ambaye ningewahi kutumainia ndani ya Yesu. Asante kwa upendo na uwepo wako wa kila siku katika maisha yangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon