Roho wa Kweli

Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli atawaongoza awatie kwenye kweli yote (YOHANA 16:13)

Nilihuzunika na kuwa na matatizo mengi katika maisha yangu, lakini kwa miaka mingi niliwalaumu watu wengine na hali zangu. Nilikuwa na muda mgumu katika kuanzisha na kuendeleza mahusiano mazuri, na nikashawishika kwamba watu wote katika maisha yangu walihitaji kubadilika ili tuelewane. Kwa kweli sikujua kwamba mimi ndiye nilisababisha shida.

Siku moja katika mwaka wa 1976, nilipokuwa ninamuombea mume wangu ili abadilike, Roho Mtakatifu alianza kuzungumza katika moyo wangu. Nilipigwa na butwaa aliponifunulia kwa upole udanganyifu niliokuwa nimejiingiza kwa kuamini kwamba kila mtu isipokuwa mimi alikuwa na shida. Kwa muda wa siku tatu, Roho Mtakatifu alinifunulia kwamba nilikuwa mgumu wa kuhusiana naye, mgumu wa kufurahisha, mwenye kukosoa, mchoyo, mwenye kutawala, mwenye kudhibiti- na huo tu ndio mwanzo wa orodha.

Kukabiliana na ukweli huu lilikuwa jambo gumu, lakini vile Roho Mtakatifu alinipa neema, nilianza safari ya uponyaji na uhuru katika maisha yangu. Ukweli mwingi ninaofundisha sasa unatokana na nyakati hizo. Shetani ndiye mdanganyifu mkubwa na baba wa uongo; iwapo anaweza kutuweka katika giza, basi anaweza kutuweka katika utumwa na dhiki. Hata ingawa kukabiliana na ukweli kunaweza kuwa na uchungu, ni muhimu kwa maendeleo na uhuru.

Vile Yesu alisema katika andiko la leo, Roho Mtakatifu ni Roho wa ukweli, na atazungumza nasi kutuongoza katika ukweli wote.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Muombe Roho Mtakatifu akufunulie maeneo yoyote ya udanganyifu katika maisha yako.  

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon