Roho wa Neema

Mtu aliyeidharau sheria ya Musa hufa pasipo huruma, kwa neno la mashahidi wawili au watatu, mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa …na kumfanyia jeuri Roho wa neema? (Waebrania 10:28-29)

Roho Mtakatifu ni Roho wa neema. Neema ni nguvu za Roho Mtakatifu za kuturahisishia kufanya chochote tunachofanya. Lakini kwanza, ni nguvu zinazotuwezesha kuwa wenye haki mbele za Mungu ndipo aweze kuishi ndani yetu na kuwa makao yake. Tukiwa na Roho Mtakatifu ndani yetu, tunaweza kufika ndani ya mioyo yetu na kuchota nguvu za Roho wa wa neema ili kufanya tusichoweza kufanya kwa kung’ang’ana katika nguvu zetu wenyewe.

Kwa mfano, nilitumia miaka yangu mingi nikijaribu kujibadilisha kwa sababu niliona kasoro nyingi katika tabia zangu. Mara nyingi nilihisi kukata tamaa kwa sababu jitihada zangu zote na kufanya kazi kwa bidii hakukuwa kunaleta mabadiliko. Nilipogundua kwamba nilikuwa nikisema vitu vibaya ambavyo sikufaa kusema, nilidhamiria kuacha, lakini kadri nilivyojaribu kubadilika ndivyo nilipozidi kuwa mbaya zaidi.

Mwishowe, nilimlilia Mungu, nikikiri kwamba nisingejaribu kubadilika zaidi. Kufikia hapo, nilimsikia Mungu akizungumza na roho yangu, “Vizuri. Sasa ninaweza kufanya kitu katika maisha yako.”

Mungu anapofanya mabadiliko hayo katika maisha yetu, Mungu anapata utukufu; kwa hivyo ataturuhusu kujibadilisha. Tukijaribu kubadilika bila kumtegemea Mungu, “tunamuacha nje.” Badala ya kujaribu kujibadilisha, tunaweza tu kumwambia atubadilishe halafu aruhusu Roho wake wa Neema kufanya kazi ndani yetu.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Usiwahi kujaribu kufanya lolote bila kuomba usaidizi wa Mungu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon