Roho wa Upendo

Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wowote. Tukipendana, Mungu hukaa ndani yetu na pendo lake limekamilika ndani yetu (1YOHANA 4:12)

Hatuwezi kutoa tusicho nacho. Kujaribu kupenda wengine ni kazi bure iwapo hatujawahi kupokea upendo wa Mungu sisi wenyewe. Tunafaa kujipenda kwa njia ya kiasi, sio kwa njia ya kibinafsi ya kujifikiria tu. Huwa ninafundisha kwamba tujipende sio kuwa katika mapenzi na nafsi zetu.

Ili kujipenda, unahitaji tu kuamini katika upendo wa Mungu juu yako; kujua kwamba ni wa milele, usiobadilika, na usio na masharti. Acha upendo wako ukuthibitishe na kukufanya uhisi usalama, lakini usianze kujinia makuu kupita inavyokupasa kunia (soma Warumi 12:3). Kujipenda hakuna maana kuwa tupende tabia zetu zote; ina maana kwamba tupende na kukubali mtu wa kipekee ambaye Mungu ametuumba kuwa.

Ninaamini kwamba kujipenda kwa kiasi ndiko hututayarisha kuruhusu upendo utiririke kutoka kwetu hadi kwa wengine. Bila kupokea upendo wa Mungu kwetu sisi binafsi kwa njia yenye afya na inayofaa, huenda tukawa na hisia za kuathiri au kuheshimu watu, aina ya upendo wa kibinadamu; lakini bila shaka hatuwezi kupenda watu bila masharti isipokuwa Mungu mwenyewe atufunulie na kuchochea upendo huo.

Roho Mtakatifu hutakasa mioyo yetu ili turuhusu upendo wa kweli wa Mungu kutiririka kupitia kwetu (soma 1 Petro 1:22) hadi kwa wengine. Hii ni sehemu moja ya kujazwa na Roho.

Mungu anataka tuonyeshe upendo kwa watu. Tunapofikiria kuhusu watu wengine na jinsi tunavyoweza kuwabariki, tunaendelea kujazwa na Roho Mtakatifu, ambaye ni Roho wa Upendo.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Una kitu kizuri cha kuupa ulimwengu leo- upendo wa Mungu ulio ndani yako.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon