Roho wa Utakatifu

Na kudhirishwa kwa uweza kuwa Mwana wa Mungu, kwa jinsi ya roho ya utakatifu, kwa ufufuo wa wafu, Yesu Kristo Bwana wetu (WARUMI 1:4) 

Andiko la leo linamrejelea Roho Mtakatifu kama “Roho wa Utakatifu.” Anaitwa kwa jina hili kwa sababu yeye ni mtakatifu wa Mungu na kwa sababu ni jukumu lake kufanya kazi ya utakatifu ndani ya kila mtu amwaaminiye Yesu Kristo kama Mwokozi.

Mungu anataka na anatuagiza tuwe watakatifu (soma 1Petro 1:15-16). Hawezi kutuambia tuwe watakatifu bila kutupatia usaidizi tunaohitaji kutufanya hivyo. Roho asiye mtakatifu hawezi kutufanya watakatifu. Kwa hivyo Mungu hututumia Roho wake katika mioyo yetu ili kufanya kazi kamilifu kabisa ndani yetu.

Katika Wafilipi 1:6, Paulo anatufundisha kwamba Mungu, aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu. Roho Mtakatifu ataendelea kufanya kazi ndani yetu mradi tu tuko hai humu duniani. Mungu anachukia dhambi, na wakati wowote anapoipata ndani yetu, anafanya kazi haraka kutusafisha kutokana nayo.

Ukweli huu peke yake unaeleza ni kwa nini tunahitaji Roho Mtakatifu kuishi ndani yetu. Yuko hapo sio tu kutuongoza na kutuelekeza katika maisha haya, lakini pia kufanya kazi mara moja kwa ushirika na Baba kuondoa chochote ambacho hakimpendezi. Atazungumza nasi kuhusu vitu ambavyo tunahitaji kubadilisha ili tuweze kukua katika utakatifu na kutuwezesha kufanya mabadiliko tunayohitaji kufanya.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Unakua katika utakatifu kwa sababu Roho wa Utakatifu anaishi ndani yako.  

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon