Sababu ya kuja kwake Yesu

Sababu ya kuja kwake Yesu

Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili. Yakobo 4:8

Nataka uone kitu kuhusu mstari hapo juu. Ona kwamba tunaambiwa kumkaribia Mungu kabla ya kuambiwa kuacha dhambi.

Kuna watu wengi ambao wanaiona kinyume. Wanafikiri hawawezi kamwe kuja kwa Mungu, hawawezi kamwe kuwa na uhusiano na Yeye, na hawawezi kamwe kuwa Wakristo kwa sababu wana matatizo katika maisha yao na kwamba wanajaribu kushinda kwanza. Wao wanajaribu kujiweka wakamilifu ili waweze kuwa wazuri wa kutosha kuwa na uhusiano na Yeye.

Lakini hiyo ni mbaya.Yesu alikuja kwa sababu hatuwezi kuwa wazuri kutosha bila Yeye. Tunapaswa kuwa na Yesu katika maisha yetu. Kifo chake, damu yake iliyomwagika kulipwa kwa ajili ya dhambi zetu-kulipiwa deni letu.

Hakuna njia tunayoweza kutakaswa dhambi mpaka tukaribie Mungu kupitia jina la Yesu. Mungu anatamani wewe uje karibu naye leo. Usijiweke mbali, uamini uongo kwamba lazima utakaswe dhambi kwanza. Badala yake, nenda kwa Mungu, na acha akusafishe kwa njia ya dhabihu ambayo Yesu alikufanyia.

OMBI LA KUANZA SIKU

Mungu, mimi naja kwako kwa njia ya damu ya Yesu inayonitakasa dhambi yangu. Asante kwa msamaha wako. Mimi nakataa kuishi kwa aibu kwa sababu najua ninaweza kukukaribia Sasa, kupokea upendo wako na msamaha.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon