Shina La Kukataliwa

Shina la Kukataliwa

Kristo akae mioyoni mwenu kupitia kwa imani [atulie, aishi, afanye makao yake) katika mioyo yenu! Muwe na shina na msingi katika upendo. —WAEFESO 3:17

Kukataliwa huanza kama mbegu ambayo imepandwa katika maisha yetu kupitia kwa vitu tofauti vinavyotutendekea. Mungu anatupenda na kutukubali, lakini shetani huiba ukweli huo kutoka kwetu kwa kutufanya tufikirie kuwa tumekataliwa kwa hivyo tunahisi kuwa tumekataliwa na kutokupendwa. Hili linapofanyika, linaathiri kila sehemu ya maisha yetu. Yanakuwa mti wenye matawi mengi yanayozaa matunda mabaya.

Chochote ulichozamia, kitaamua tunda litakalokuwa katika maisha yako—zuri au baya. Iwapo umezama katika kukataliwa, dhuluma, aibu, kuhukumika, au kuwa na picha mbaya kujihusu—iwapo umezama katika kufikiri, Kuna kitu kibaya kunihusu!— “mti” wako utazaa mfadhaiko, uhasi, kukosa matumaini, hasira, uadui, roho wa kudhibiti, kuhukumu, chuki na kujihurumia. Ikiwa umezama ndani ya Yesu na katika upendo wake, unaweza kupumzika na kujua kwamba unapendwa na una thamani. Unaweza kujua kuwa Mungu anakuona kama asiye na kosa kupitia kwa imani yako ndani ya Yesu.

Sehemu zote za maisha yako ambazo zina kasoro zinaweza kurekebishwa kupitia kwa Yesu na kazi aliyofanya msalabani. Ilifanyika kwangu na Mungu anaweza kukufanyia wewe.


Hizi hapa habari njema—unaweza kuwekwa huru kutokana na nguvu za kukataliwa!

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon