Shiriki na Bwana

Shiriki na Bwana

Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote. YEREMIA 29:13

Hata tukajifunza kanuni na fomula ngapi, hatutawahi kuwa na ushindi wa kudumu katika maisha yetu ya ukristo bila kutenga muda kuwa na Bwana katika ushirika wa kibinafsi wa kisiri. Ushindi haupo katika mbinu; uko ndani ya Mungu. Iwapo tunataka kuishi kwa ushindi, itabidi tukiuke kutafuta njia za kukatisha shida zetu na kumpata Yesu katikati ya shida zetu.

Habari njema ni kwamba tunapotenga muda kuwa na Mungu, anakutana nasi. Tunaweza kuwa wenye shukrani tukijua kwamba, tukimtafuta, tutampata. Mungu ana mpango binafsi kwa kila mmoja wetu, mpango ambao utatuongoza hadi kwa ushindi. Ndiyo kwa sababu kanuni, fomula na mbinu sio jibu la mwisho, kwa sababu haziruhusu watu kuwa na tofauti za kibinafsi. Hivi vitu vinaweza kuwa vizuri tu kama mwongozo wa kijumla lakini sio vibadala vya ushirika wa kibinafsi na Mungu aliye Hai.


Sala ya Shukrani

Asante, Baba, kwamba ninaweza kukutana nawe wakati wowote wa mchana au usiku. Uko hapa kila wakati kwa ajili yangu na unatamani kutumia muda kuwa nami. Neno lako linasema nikikutafuta, nitakupata. Kwa hivyo nisaidie, Bwana, kukupata katika kila sehemu ya maisha yangu leo.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon