Shukrani Kwa Kemeo la Mungu

Shukrani Kwa Kemeo la Mungu

Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu. Ufunuo Wa Yohana 3:19 Biblia

Mungu hutazama uhakikisho, kemeo na nidhamu kama vitu vya kusherehekewa badala ya vitu vya kutukasirisha au kutufadhaisha. Kwa nini tunafaa kusherehekea Mungu anapotuonyesha kwamba kuna kitu kibaya nasi? Ni kwa sababu ni habari njema kwetu anapotufungua macho kuona kitu ambacho wakati mmoja hatukuwa tukikiona.

Tukipiga hatua za kutosha katika uhusiano wetu na Mungu kiasi cha kuanza kuhisi tunapokuwa nje ya mapenzi yake, basi hicho ni kitu cha kushukuru kwacho. Ni ishara ya maendeleo na inafaa kusherehekewa kwa furaha. Kadri tunavyomtumikia Mungu na kusoma njia zake, ndivyo tunavyovutiwa kujua mapenzi yake. Hatimaye tunakua hadi mahali ambapo tunaanza kujua mara moja iwapo tunafanya au kusema kitu kisichompendeza Mungu, na tunaweza kuchagua kutubu na kuwa na mwanzo mpya.


Sala ya Shukrani

Ninashukuru, Baba, Kwamba unanipenda vya kutosha hata kuleta kemeo na maagizo katika maisha yangu. Asante kwamba unanigeuza na kunifanya nifanane zaidi na Mwanao Yesu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon