Sikati Tamaa

Sikati Tamaa

Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu. [Niko tayari kufanya lolote na kuweza lolote kupitia yeye anitiaye nguvu; ninajitosheleza katika utoshelevu wa Kristo]. —WAFILIPI 4:13

Mara nyingi, watu huja kwangu kwa ushauri na maombi, na ninapowaambia vile Neno la Mungu linavyosema, au ninachofikiria kuwa Roho Mtakatifu anasema, jibu lao huwa, “Ninajua ni sawa; Mungu amekuwa akinionyesha jambo hilohilo. Lakini, Joyce, ni vigumu tu sana.” Hiki ni kimojawapo cha visingizio vingi ninavyosikia kutoka kwa watu.

Mwanzoni nilipoanza kusoma Neno la Mungu kuhusu vile ningefanana zaidi na Yesu, halafu nikalilinganisha na mahali nilipokuwa, pia mimi nilisema, “Ninataka kufanya mambo unavyofanya, Mungu, lakini ni vigumu sana.” Mungu kwa neema akanionyesha kuwa huu ni uongo ambao adui hujaribu kutia katika mawazo yetu ili tukate tamaa. Lakini sheria za Mungu si ngumu sana kwetu kufuata tukizifuata kupitia kwa nguvu za Kristo. Kutembea katika utiifu kwa Mungu si vigumu sana kwa sababu ametupatia Roho wake ili afanye kazi ndani yetu kwa nguvu na kutusaidia kufanya mambo aliyotuambia tufanye (Yohana Mtakatifu 14:16). Yuko ndani yetu, pia nasi kila wakati ili kutuwezesha kufanya tusiyoweza kufanya, na kufanya kwa urahisi yanayoweza kuwa magumu bila Yeye!


Mambo huwa magumu tunapojaribu kuyafanya peke yetu bila kuegemea au kutegemea neema ya Mungu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon