Sikia Mungu Kupitia kwa Neno Lake

Umthibitishie mtumishi wako ahadi yako, inayohusu kicho chako (ZABURI 119:38)

Mungu huzungumza nasi kupitia kwa Neno lake na Neno lake limepangwa kutusaidia, kutuelekeza, na kutuhimiza katika maisha yetu ya kila siku. Tunaweza kusikia sauti ya Mungu katika kila hali, kwa sababu tunaweza kupata maandiko au mistari tofauti ya kutumia kwa maombi katika kila hali. Wakati mwingine, maandiko au mistari ya Biblia hutupatia maelekezo maalum yenye kina. Wakati mwingine tunahitaji kuchukua kipande cha hekima au kanuni ya jumla ya kiroho na kuitumikisha kwa jambo tunaloshughulikia. Kwa mfano, hii hapa orodha ya baadhi ya hali na hisia maalum za kawaida ambazo adui hutumia kututishia na maandiko yanayokubaliana nazo ambayo tunaweza kutumia katika maombi yetu:

  • Unapopitia kwa msimu wa matatizo au kitu ambacho kinakuchosha, unaweza kuomba Isaya 40:29: “Huwapa nguvu wazimiao, humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo.”
  • Unapokuwa na wasiwasi kuhusu mstakabali, unaweza kuomba Yeremia 31:17, ambayo inasema, “Tena liko tumaini kwa siku zako za mwisho.”
  • Unapong’ang’ana kifedha, unaweza kuomba Zaburi 34:9-10, “Mcheni Bwana, enyi watakatifu wake, yaani wamchao hawahitaji kitu. Wana-simba hutindikiwa, huona njaa, bali wamfuatao Bwana hawahitaji kitu chochote kilicho chema.”

Kwa kweli ninaamini kwamba Neno la Mungu lina jibu la kila swali tulilonalo na hekima ya kukutana na kila hitaji.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Hisia zinaweza kutupotosha, lakini Neno la Mungu hutuongoza kwenye usalama.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon