Hata imekuwa, mtu akiwa [amepandikizwa] ndani ya Kristo [Masiya] amekuwa kiumbe kipya! [kiumbe kipya kabisa] Ya kale [hali ya kale ya kitabia na kiroho] yamepita tazama! Yamekuwa mapya! —2 Wakorintho 5:17
Kama “kiumbe kipya” si lazima uruhusu mambo ya kale yaliyokufanyikia kuendelea kuathiri maisha yako mapya katika Kristo. Wewe ni kiumbe kipya na maisha mapya katika Kristo. Unaweza kugeuzwa nia yako kulingana na Neno la Mungu. Mambo mema yataenda kukufanyikia!
Anza kuwa na fikra chanya kuhusu maisha yako. Hiyo haimaanishi kwamba unaweza tu kupata kitu chochote unachotaka tu kwa kukifikiria. Mungu ana mpango mtimilifu kwa kila mmoja wetu, na hatuwezi kumdhibiti kwa mawazo yetu na maneno. Lakini ni muhimu kwetu sisi kuwaza na kuzungumza kulingana na mapenzi yake na mpango wake juu ya maisha yetu.
Iwapo huna habari kuhusu mapenzi ya Mungu juu yako kufikia hapa, unaweza kuanza kwa kuwaza namna hii—sawa, sijui mpango wa Mungu, lakini ninajua ananipenda. Chochote atakachofanya kitakuwa kizuri, na nitabarikiwa.
Mungu ameanza kazi nzuri ndani yako na ataikamilisha (Wafilipi 1:6). Kwa hivyo hata ukijisikia kukata tamaa kwa sababu hupigi hatua upesi, kila mara kumbuka kwamba Mungu anafanya kazi ndani yako na hatakuacha wala kukupungukia.
Yesu atakuweka huru ili ufurahie vitu vizuri katika maisha. Amini Mungu kukugeuza nia yako kwa Neno lake!