
Nami nikatafuta mtu miongoni mwao, atakayelitengeneza boma, na kusimama mbele zangu mahali paIipobomoka, kwa ajili ya nchi, nisije nikaiharibu, lakini sikuona mtu (EZEKIELI 22:30)
Pengo ni uwazi kati ya vitu viwili; infanya vitu, uwazi, chombo, au watu wawili kuingiana. Ninapohubiri katika nchi za kigeni, kuna pengo kati yangu na hadhira. Kunaweza kuwa na pengo katika jukwaa; kunaweza kuwa na pengo la kiutamaduni, lakini ninakuwa na wasiwasi kuhusu pengo la lugha. Ninapotaka watu kunielewa, huwa nahitaji mkalimani, mtu wa kusimama katika pengo la lugha kwa niaba yangu ili niwasilishe ujumbe kwa njia muafaka. Mkalimani huyo atafanya kazi kwa niaba yangu ndiyo pengo liweze kuondolewa na watu waelewe ninachosema.
Ezekieli 22:29–31 inasema kuhusu kusimama katika pengo. Andiko la leo linapatikana katika aya hiyo na ni mojawapo ya maelezo ya huzuni katika Biblia. Ndani yake, Mungu kimsingi alikuwa anasema, “Nilihitaji mtu kuomba, lakini sikuweza kupata mtu aliyeweza kufanya hivyo, kwa hivyo ikalazimu niharibu nchi.” Walichohitaji alikuwa mtu mmoja kuomba, na nchi yote isingeharibiwa. Je, unaona jinsi uombezi ulivyo muhimu? Mtu mmoja peke yake angeleta tofauti katika nchi nzima na kuokoa nchi nzima kupitia kwa maombi! Tunahitaji kuhiari kuomba; tunahitaji kuwa wahisivu na watiifu kwa zile nyakati ambazo Roho Mtakatifu hutuongoza kuombea watu. Hatuwezi kujua wakati ambao maombi yetu yanaweza kuwa yanahitajika kujaza pengo na kuunganisha nguvu za Mungu na hali ya kukata tamaa.
NENO LA MUNGU KWAKO LEO:
Mwambie Mungu upo kuombea wengine na ufanye hivyo anapoweka watu mbalimbali kwenye moyo wako.