Tafakari kuhusu Mambo ya Mungu

Tafakari kuhusu Mambo ya Mungu

. . . Yoyote yaliyo ya kweli, yoyote yaliyo ya staha, yoyote yaliyo ya haki, yoyote yaliyo safi, yoyote yenye kupendeza, yoyote yenye sifa njema, ukiwapo wema wowote, ikiwapo sifa nzuri yoyote, yatafakarini hayo… —WAFILIPI 4:8

Ulijua kuwa hisia zako zinaambatana na mawazo yako? Iwapo unafikiri si kweli, hebu chukua tu takriban dakika ishirini na usifikirie kuhusu kitu kingine isipokuwa shida zako. Ninaweza kukuhakikishia kuwa kufikia mwisho wa wakati huo, hisia zako, na pengine sura yako itakuwa imebadilika.

Siku moja niliamka nikifikiri kuhusu shida ambayo nilikuwa nayo. Mara tu Roho wa Bwana akazungumza nami. Akasema, “Joyce, utakuwa na ushirika nami au shida yako?”

Unaposikitika, usikae hapo na kujionea huruma. Hata kama mambo ni magumu vipi, tunaweza kufanya uteuzi. Tunaweza kuchagua kuwa katika uhusiano wa karibu na shida zetu au kuwa katika uhusiano wa karibu na Mungu. Tunaweza kuruhusu mawazo yetu kuzama katika shida zetu hadi tukakata tamaa kabisa na kuvunjika au tunaweza kulenga umakini wetu kwenye vitu vyote vizuri ambavyo vimewahi kufanyika katika maisha yetu—na kwa baraka zote ambazo Mungu ametuwekea katika siku zijazo.


Mawazo yetu ni maneno tuli ambayo Mungu na sisi peke yetu ndio huyasikia, lakini maneno hayo huathiri mtu wetu wa ndani, afya yetu, furaha yetu na mielekeo yetu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon