Tafuta Mpaji, Sio Kipaji

Tafuta Mpaji, Sio Kipaji

Mtafuteni Bwana, maadamu anapatikana, mwiteni maadamu yu karibu. ISAYA 55:6

Mojawapo ya vitu vingi ambavyo tunafaa kushukuru kwacho katika uhusiano wetu na Mungu ni kwamba anataka kuwa rafiki yetu (tazama Yohana 15:15). Lakini unapokua katika urafiki wako na Mungu, usiwahi kusahau kwamba uhusiano wenu unamtegemea Yeye jinsi alivyo na sio kile anachoweza kukufanyia. Endelea kutafuta uwepo wake sio zawadi zake.

Mojawapo ya vizuizi vya uhusiano wa mkomavu wa kusisimua na Mungu ni kutazama faida za urafiki wetu na Mungu badala ya kumtazama kama rafiki yetu. Kama wanadamu, hatushughuliki kutambua kwamba watu fulani wanataka kuwa marafiki zetu tu kwa sababu tunaweza kuwapa kitu wanachotaka; tunahisi kuthaminiwa tunapojua kwamba watu wanataka urafiki nasi tu kwa sababu ya jinsi tulivyo na kwa sababu wanatupenda—kanuni hiyo inatumika kwa Mungu pia.


Sala ya Shukrani

Ninakushukuru Mungu, kwamba unanipenda na unataka kuwa katika uhusiano nami. Leo, ninakutafuta kwa ajili ya jinsi ulivyo, sio kwa sababu ya kile unaweza kunifanyia. Ni hamu ya moyo wangu kukujua zaidi na zaidi kila siku ninayokufuata.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon