Tazama Umbali Uliokuja

Ili kwamba kujaribiwa kwa imani yenu, ambayo ina thamani kuu kuliko dhahabu ipoteayo, ijapokuwa hiyo hujaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa wenye sifa na utukufu na heshima, katika kufunuliwa kwake Yesu Kristo. —1 PETRO 1:7

Kuna majaribu mengi ambayo hutupata kila siku. Kwa mfano, mkubwa wetu kazini anatwambia kufanya kitu tusichotaka kufanya. Au tunaenda kuegesha gari nafasi fulani maegeshoni na mtu anaendesha gari na kuliegesha hapo. Au mtu anatuzungumzia kwa ujeuri baada ya kumtendea kitu.

Katika 1 Petro 4:12, Petro anatuambia tusishangae na kuduwaa kwa mitihani ambayo lazima tuvumilie kwa sababu, kwa mitihani hiyo, Mungu anajaribu “ubora” wetu, au hulka yetu. Petro alijua thamani ya kujaribiwa katika maisha yake mwenyewe. Sisi sote hupitia katika mitihani hiyo na hatufai kuchanganyikiwa na kujiuliza ni kwa nini inafanyika. Mioyo yetu inajaribiwa ili kuthibitisha hulka yetu.

Kila wakati Mungu anapotupatia mtihani, tunaweza kujua umbali tuliotoka na umbali ambao bado tunaenda kwa jinsi tunavyokabiliana na mtihani huo. Nia za moyo ambazo hata hatukujua tunazo zinaweza kudhihirika tunapokuwa katika mitihani na majaribu. Hiki ni kitu kizuri kwa sababu hatuwezi kufika tunapohitaji kuwa tusipotambua mahali tulipo.


Kila kitu ambacho Mungu anaruhusu katika maisha yetu ni kwa sababu ya wema wetu, hata kama huhisi vizuri wakati huo.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon