Tazama Umbali Uliotoka

Tazama Umbali Uliotoka

Lakini sasa, Ee Bwana, wewe u baba yetu; sisi tu udongo, nawe u mfinyanzi wetu; sisi sote tu kazi ya mikono yako. ISAYA 64:8

Ni rahisi sisi kuanza kufikiria umbali ambao tutaenda katika kufikia malengo yetu badala ya kusherehekea umbali ambao tumetoka.Fikiria kuhusu hilo. Umetoka umbali gani tangu uwe Mkristo? Umebadilika kiasi gani? Unafurahia kiasi gani? Una amani zaidi kuliko vile ulivyokuwa awali? Una tumaini? Huwa kuna mengi ya kusherehekea tukiyatafuta.

Tukisoma Biblia kwa makini, inaonyesha kwamba mara nyingi, wanaume na wanawake ambao Mungu alitumia kwa njia kuu walikuwa na moyo wa kusherehekea kile ambacho Mungu alifanya. Hawakupuuuza wema wake, lakini kwa uwazi walionyesha furaha na shukrani kwa vitu vidogo na pia vikubwa.


Sala ya Shukrani

Baba, leo ninachagua kuwa mwenye shukrani tele kwa sababu ya umbali ambao umenileta. Huenda nisiwe mahali ninapotaka kuwa, lakini ninakushukuru kuwa siko mahali nilipokuwa.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon