Thawabu ya Kutoa Upendo

Thawabu ya Kutoa Upendo

Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi. —YOHANA 13:35

Mojawapo ya njia nzuri za kuupa Yesu ulimwengu ni kuwaonyesha tu wengine upendo. Yesu mwenyewe alifundisha kuhusu upendo na akatembea katika upendo, kwa sababu hicho ndicho ulimwengu unahitaji. Ulimwengu unahitaji kujua kwamba Mungu ni upendo na anampenda kila mtu bila masharti (1 Yohana 4:8).

Neno la Mungu linafundisha pia kwamba Mungu anatutaka tujitolee kujenga hulka ya Yesu Kristo katika maisha yetu binafsi halafu twende nje kama wajumbe wa Kristo kwa ulimwengu (2 Wakorintho 5:20).

Ili kuwa wajumbe wake, ni muhimu kugeuzwa nia zetu ili tuelewe upendo unamaanisha nini. Upendo sio tu hisia tulio nayo; ni uamuzi wa kutendea watu vile Yesu angewatendea.

Kwa kweli tukijitolea kutembea katika upendo, itasababisha madadiliko makubwa katika mtindo wetu wa maisha wakati wote. Njia zetu nyingi—mawazo yetu, mazungumzo yetu, desturi zetu—zinahitaji kubadilika. Upendo hushikika; huonekana kwa mtu yeyote anayekumbana nao.

Kupenda wengine hakuji kwa urahisi au bila dhabihu ya kibinafsi. Kila wakati tunapochagua kumpenda mtu, itatugharimu kitu—wakati, hela, au bidii. Lakini thawabu ya kuwapenda wengine ni zaidi ya gharama ilivyo.


Kupenda wengine hakutegemei hisia zetu; ni uteuzi tunaofanya.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon