Tii Neno

Tii Neno

Lakini iweni watendaji wa neno, wala wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu. —YAKOBO 1:22

Ninamkumbuka mwanamke aliyehudhuria mojawapo ya warsha zangu. Alitaka kwa vyovyote kuwekwa huru kutokana na vidonda vya kihisia ambavyo vilikuwa vimemwacha bila usalama na mwingi wa hofu, lakini hakuna kilichomwendea vizuri. Baada ya kuhitimisha warsha, aliniambia kwamba sasa alifahamu ni kwa nini alikuwa hajawahi kuwa na maendeleo yoyote.

Akasema, “Joyce, nilikaa na kikundi cha wanawake ambao walikuwa na matatizo mengi kama niliyokuwa nayo. Hatua kwa hatua Mungu alikuwa akiwaweka huru. Nilipokuwa nikisikiliza, nilisikia wakisema, “Mungu ameniongoza kufanya hiki, na nilifanya. Halafu akaniongoza kwa kitu kingine, na nikakifanya.” Nikatambua kuwa Mungu alikuwa ameniambia kufanya vitu hivyo hivyo pia. Tofauti ni kuwa walifanya alichowaambia kufanya, nami sikufanya.”

Kuishi katika uhusiano wa karibu na Mungu na kupokea anayoahidi, lazima tutii Neno la Mungu. Tunafaa kuwa watendaji wa Neno na sio tu wasikiaji. Kutii Neno huhitaji uzoefu na bidii. Hebu tujitie wakfu na kujitolea kufuata uongozi wa Mungu.


Njia ya Mungu hufanya kazi! Na hakuna njia nyingine inayoweza. Fanya uamuzi wa kimaksudi kutii Neno lake hatua baada ya nyingine, kila siku.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon