Tunachokijua (Sehemu ya 2)

Tunachokijua (Sehemu ya 2)

Ili kwamba ushirika wa imani yako ufanye kazi yake, katika ujuzi wa kila kitu chema kilicho kwetu katika Kristo. FILEMONI 1:6

Unapojua ukweli wa kimaandiko ufuatao, huwezi kuacha kuwa na shukrani…

Tumefanywa viumbe vipya ndani ya Kristo, ya kale yamepita na vitu vyote vimekuwa vipya mno. Tunaweza kusahau makosa ya zamani na kuchuchumilia mbele kwenye utimilifu. Tunajua kuwa Mungu anatupenda kwa upendo wa milele, upendo usio na masharti, na kwamba rehema zake hudumu milele. Tunajua kwamba mambo yote yanawezekana kwake Mungu na tunaweza kufanya mambo yote kupitia kwa Kristo aliye nguvu zetu.

Tunajua kwamba Mungu huwa haruhusu tujaribiwe kupita tuwezavyo, hufanya mlango wa kutokea wakati wote, mahali salama pa kutua. Tunajua kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani wale walioitwa kulingana na kusudi lake, na kwamba kile maadui zetu walikusudia kitudhuru, Mungu anakikusudia kwa mema. Tunajua kwamba yeye ni Mtetezi wetu, Mkombozi wetu, na Mrejeshi. Hufanya upya vitu vyote!


Sala ya Shukrani

Baba, ninaomba kwamba hayo maneno hayatakuwa tu kitu nilichosoma, lakini yataota mizizi ndani kabisa ya moyo wangu. Asante kwa ahadi zako. Ninaziamini na kuchagua kukaa ndani yake leo na kila siku kwenda mbele.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon