Tunafanya Kazi Pamoja

Kwa kuwa kama vile katika mwili mmoja tuna viungo vingi, wala viungo vyote havitendi kazi moja, vivyo hivyo na sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na viungo kila mmoja kwa mwenzake (WARUMI 12:4-5)

Maandiko ya leo yanatufundisha kuhusu utofauti wa karama zinazopewa kila mtu binafsi. Sisi wote ni viungo tofauti vya mwili mmoja wa Kristo , naye ndiye kichwa. Katika ulimwengu wa kimwili, lazima viungo vyote vya mwili vihusiane na kichwa iwapo kila kitu kitakuwa na mpangilio mzuri wa kazi. Viungo tofauti vya mwili hufanya kazi pamoja; havina wivu wala kushindana. Mikono husaidia miguu kuvaa viatu. Miguu hupeleka mwili popote unapohitaji kwenda. Mdomo huzungumza kwa niaba ya mwili mzima. Kuna viungo vingi sana vya mwili; vyote havifanyi kazi moja, lakini vyote hufanya kazi pamoja kwa kusudi moja. Mwili wa kirohoo wa Yesu unafaa kufanya kazi vivyo hivyo. Ndiyo kwa sababu Roho Mtakatifu alitumia mfano wa mwili wa binadamu alipomchochea Paulo kuandika kitabu cha Warumi.

Tunapojaribu kufanya kazi kwa njia yoyote ile isipokuwa ile ambayo Mungu amebuni na kutupangia tufanyie kazi, tunaishia kuwa na shinikizo katika maisha yetu. Lakini tukifanya kile ambahco Mungu ametupangia kufanya, tunakuwa na furaha, kuridhika na tuzo kubwa. Tunahitaji kufanya kazi na Roho Mtakatifu ili kugundua kudura yetu binafsi ya kipekee, halafu tufanye kila tuwezalo kuitimiza. Mungu anapokupa karama ya kitu fulani au kukuwezesha kufanya kitu, utakifanya vizuri sana, kwa hivyo tafuta kitu unachofanya vizuri na uanze kukifanya.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Unapotaka kutumiwa na Mungu, basi tafuta haja na ukutane nayo.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon