Tunda la Milele

Kama vile Baba alivyonipenda mimi, nami nilivyowapenda ninyi, kaeni katika pendo langu (YOHANA 15:9)

Sitawahi kusahau wakati ambao Dave aliamua kwamba mti mkuu uliopendeza ambao ulikuwa nje ya nyumba yetu ulihitaji kupunguzwa. Ulikuwa na matawi yaliyovurugika na ulikuwa umeanza kuning’inia upande mmoja. Sikuwaza sana kuhusu hilo aliposema kwamba angeleta wataalamu wa kufanya kazi hiyo ya kuupunguza na kuufanya uwe mwembamba. Lakini nilishangaa nilipofika nyumbani na kupata kwamba hao wanaume wanaofurahia kufanya kazi na misumeno walikuwa wameuhujumu mti wangu.

Dave akasema, “Ngoja tu mpaka mwaka ujao, utakuwa wa kupendeza tena.” Lakini sipendi kungoja.

Na sipendi kuangalia mabaki ya kichokoa meno ambacho kilistawi na kujaa wakati mmoja. Lakini Dave alisema ukweli. Mwaka uliofuatia, mti ulipendeza kuliko ulivyokuwa, ukaimarika kiasi cha kustahimili pepo zenye nguvu kwa kipindi cha miaka mingi, na kuwa wenye kuzalisha matunda milele. Huu ni mfano mtimilifu wa kazi ya kupunguza ya Roho Mtakatifu katika maisha yetu- na kupunguza kwake huleta matokeo ya  urembo, nguvu na uzalishaji ndani yetu.

Wagalatia 5 inatupatia orodha ya dhambi za mwili na orodha ya tunda la Roho, na ni muhimu kwa mwili kupunguzwa kila mara ili kuandaa nafasi ya tunda zuri zaidi na zaidi. Kama vile mti wangu, wakati mwingine tunaning’inia upande mmoja au kutokuwa na kiasi na lazima Mungu atushughulikie ile atunyoshe kabisa tena. Tunafaa kuwa na shukrani kwamba Mungu anatujali kiasi cha kututazama na kutusaidia kuwa wazuri tuwezavyo. Mwombe Mungu aje katika maisha yako na vifaa vyake vya kukupunguza kila mara ili uweze kuzalisha matunda mema zaidi.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Adhabu haifurahishi, lakini huwa tunafurahia tunda lake baadaye. 

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon