Ufanisi wa Kweli

Ufanisi wa Kweli

Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako kama vile roho yako ifanikiwavyo. 3 YOHANA 1:2

Mtu hawi na mafanikio iwapo vitu alivyo navyo ni vitu na pesa; ufanisi wa kweli huhitaji zaidi ya hayo. Biblia inatupatia mtazamo mkamilifu kuhusu mafanikio nasi pia tunapaswa kuwa na mtazamo huo huo.

Miili yetu inapofanikiwa, tunakuwa na nguvu na wenye afya ya mwili. Hata kama tuna ugonjwa mwilini, tunaweza kuomba na kutarajia Mungu kutusaidia. Mafanikio ya kweli hujumlisha amani ya moyo na ridhia. Nafsi zetu zikifanikiwa, tunanawiri ndani. Tuna amani; tuna furaha tele; tunaishi kwa kusudi; tunakua kiroho; na tuna uhusiano wenye nguvu na upendo na watu wengine.

Yesu alisema kwamba alikuja ili tukawe na uzima tele tele (tazama Yohana 10:10). Mungu ni Mungu wa vingi, na ataka tuishi maisha yanayofurika na kujaa shukrani na furaha.


Sala ya Shukrani

Ninakushukuru Baba, kwamba unanawirisha mwili na nafsi yangu. Leo ninaomba amani na afya ambayo unaahidi katika Neno lako. Asante kwamba nimefanywa mkamilifu ndani yako.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon