Ufunguo wa Kujikubali

Ufunguo wa Kujikubali

Kwa kuwa hatuthubutu kujihesabu pamoja na baadhi yao wanaojisifu wenyewe, wala kujilinganisha nao; bali wao wenyewe wakijipima nafsi zao, na wakijilinganisha nafsi zao na nafsi zao, hawana akili. 2 WAKORINTHO 10:12

Kutangaza mara nyingi husudiwa kufanya watu waonekane bora zaidi, wawe bora zaidi, na kumiliki vitu vingi. Ukinunua “hili” gari, utakuwa nambari moja kweli! Ukinunua aina “hii” ya nguo, utakuwa tu kama “huyu” mtu maarufu na watu watakustaajabia. Kila mara ulimwengu utafanya tufikirie kwamba tunahitaji kuwa kitu kingine zaidi ya vile tulivyo.

Ujasiri huanza na kujikubali—jambo ambalo huwezeshwa kupitia kwa imani ya nguvu katika upendo na mpango wa Mungu juu ya maisha yetu. Ninaamini ni dharau kwa Mungu tunapojilinganisha na watu wengine na kutamani kuwa kama wao. Fanya uamuzi kushukuru kwa jinsi Mungu alivyokuumba, halafu hutawahi kujilinganisha na mtu mwingine tena. Furahia watu wengine jinsi walivyo na ufurahie vile ulivyo mtu wa ajabu.


Sala ya Shukrani

Baba, nisaidie kupenda na kufurahia mtu uliyeniumba kuwa. Ninakushukuru kuwa sihitaji kujilinganisha na watu wengine ili nikubalike. Uliniumba kwa kusudi la ajabu na la kipekee. Ninashukuru kwamba, kwako, mimi ni spesheli na nisiyelinganishwa.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon