
Wakashangaa mno kwa mafundisho yake; kwa maana alikuwa akiwafundisha kama mwenye umri, wala si kama waandishi. MARKO 1:22
Ni huzuni kufikiria kwamba watu wengine wanafananisha Ukristo tu na kwenda kanisani na sio kitu kingine zaidi. Kanisani tunafundishwa kuhusu Mungu, lakini shukuru kwamba maisha yetu ndani ya Kristo ni zaidi ya safari ya kila wiki ya kwenda kanisani. Kuwa Mkristo ni zaidi ya kujiunga na kanisa. Ni uhusiano wa kibinafsi na Mungu kupitia kwa Yesu Kristo.
Ili kwa kweli kumjua Bwana, lazima tuwe na njaa ya aina ya maarifa ambayo yanaweza kutoka tu kwa Mungu kupitia kwa ufunuo—ufunuo huu upo kupitia kwa Neno lake na kwa Roho Mtakatifu wake kwa njia ya uhusiano wa kibinafsi na wa ndani.
Ufunuo huenda zaidi ya tunayoyafikiria, kuona au kuhisi. Ni ujuzi wa Mungu kwa ndani kiasi cha kwamba hakuna anayeweza kuuchukua kutoka kwetu. Tunapokuwa na huu ujuzi wa Mungu wa ndani, tunaweza kushukuru na kuwa salama, tukijua kwamba hakuna kitu cha kutoka nje kinaweza kutuondoa kwa imani yetu ndani ya Mungu.
Sala ya Shukrani
Ninashukuru, Baba, kwamba ninaweza kuwa na uhusiano wa kibinafsi ulio wa ndani nawe. Leo ninachagua kusikiza sauti yako na kufuata uongozi wako. Asante kwa ufunuo wako maishani mwangu.