Ujasiri Na Utiifu

Ujasiri na Utiifu

Baada ya mambo haya neno la Bwana likamjia Abramu katika njozi likinena, usiogope, Abramu, mimi ni ngao yako, na thawabu yako kubwa sana. —Mwanzo 15:1

Katika Mwanzo 12:1, Mungu alimpa Abramu amri ngumu. Kwa maneno alisema, “Funganya na uondoke, uache kila mtu unayemjua na kila kitu ulichozoea na uende mahali nitakapokuonyesha.”

Kama Abramu angeshuku na kutokuwa na hakika, kisa kilichofuatia kisingetimia. Asingemwona Mungu kama ngao yake, fidia yake kuu, na asingepokea thawabu yake kuu ya kupindukia mipaka.
Kwa njia hiyo moja, kama Yoshua asingeshinda hofu yake na kutii amri ya Mungu ya kuongoza watu wake katika Nchi ya Ahadi, yeye mwenyewe pamoja nao pia wasingefurahia mambo yote ambayo Mungu alikuwa amewapangia na kuwatayarishia.

Kuna nguvu katika Neno la Mungu kutuhami kukoma kuzimia katika hofu kuu la kukosa uhakika. Tunaweza kufanya kile Mungu anataka tufanye, hata kama italazimu tufanye tukiwa tumeogopa. Tunapoogopeshwa na kikwazo, tunaweza kusema: “Bwana, nitie nguvu. Hili ndilo uliloniambia nifanye, na kwa usaidizi wako, nitalifanya, kwa sababu ni ufunuo wa mapenzi yako juu yangu. Nimekusudia kwamba maisha yangu hayatatawaliwa na hofu lakini kwa Neno lako.”


Mungu huwa hatuokoi “kutokana” na vitu; mara nyingi “hupitia” nasi ndani.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon