Jeshi lijapojipanga kupigana nami, moyo wangu hautaogopa; vita vijaponitokea, hata hapo nitatumaini. —ZABURI 27:3
Nimegundua kwamba kuwa na ujasiri kuhusu vile Mungu alituumba tuwe ni ufunguo wa kuishi maisha ya furaha tele, na ushindi ambayo Yesu alikufa kutupatia.
Mara nyingi shetani anajaribu kuanzisha mawazo katika akili zetu kutufanya tupoteze ujasiri wetu. Mawazo ni uwanja wa vita, na shetani hutudanganya kupitia kwa mawazo mabaya. Hujaribu kutuambia sisi si wazuri vya kutosha, tumefanya makosa mengi sana, Mungu ana hasira nasi—wazo lolote ambalo litatufanya tushuku upendo wa Mungu juu yetu. Tukitafakari juu ya hayo mawazo mabaya, ujasiri wetu unafifia.
Ufunguo wa kushinda vita vya kimawazo, ni kupigana dhidi ya uongo wa adui na ukweli wa Neno la Mungu. Huna lazima ya kuwa na mawazo mabaya; badala yake, unaweza kuamini ahadi za Mungu na kukiri ahadi hizo juu ya maisha yako kwa ujasiri.
Ninakuhimiza kukiri kwa ujasiri kile Neno la Mungu linasema kuhusu maisha yako, kama vile: “Lakini katika mambo hayo yote, tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda (Warumi 8:37). Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu (Wafilipi 4:13). Ila Mungu apewe shukrani, anayetushangiliza daima katika Kristo, na kuidhihirisha harufu ya kumjua yeye kila mahali kwa kazi yetu (2 Wakorintho 2:14).”
Shetani anapojaribu kukudanganya, kiri ukweli wa Neno la Mungu kwa ujasiri juu ya maisha yako.