Umuhimu wa Imani

Umuhimu wa Imani

Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao. Waebrania 11:6

Imani ni kani ya nguvu ambayo tunaweza kufikia na tunafaa kushukuru kwayo. Tunapoishi kwa imani, tunamwachilia Mungu kutufanyia vitu vya ajabu na kupitia ndani yetu. Imani ni kuegemeza nafsi yote ya binadamu juu ya Mungu katika uhakika kamili ndani ya nguvu, hekima na wema wa Mungu (tazama Wakolosai 1:4). Tunaweza kuja kwa Mungu kwa imani kama ya mtoto, tukiamini tu Neno lake na kuweka imani yetu ndani yake kwamba atafanya alichoahidi kufanya.

Watu wengine husema kwamba hawana imani, lakini si ukweli. Sisi wote tuna imani, lakini huenda tukachagua kutoiweka ndani ya Mungu. Unapokaa kitini, huwa una imani kwamba hakitakuangusha. Unapoweka pesa ndani ya benki huwa una imani kwamba utaweza kurudi kuzichukua utakapozihitaji. Je, wewe unaweka imani yako katika kitu gani au mtu gani?

Ninakusihi kutoweka imani yako katika kitu kisicho na uthabiti na udhaifu, lakini iweke ndani ya Mungu ambaye ni Mwamba imara na usiobadilika. Ni mwaminifu na atafanya anayoahidi kufanya wakati wote.


Sala ya Shukrani

Baba, ninashukuru kwamba umenipa kiasi cha imani. Ninaachilia imani yangu ndani yako na kuamini kwamba utatimiza mahitaji yangu wakati wote na kunishughulikia. Asante kwa wema na upendo wako.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon