Lakini mimi nawaambia iliyo kweli yawafaa ninyi, mimi niondoke, kwa maana mimi nisipoondoka, huyo msaidizi hatakuja kwenu; bali nikienda zangu, nitampeleka kwenu. —YOHANA 16:7
Lo! ingekuwa ajabu ilioje kama ningetembea na Yesu alipokuwa ulimwenguni. Lakini aliwaambia wanafunzi wake kwamba ingekuwa bora zaidi kwao iwapo angeenda, kwa sababu hivyo angemtuma Roho wake kukaa katika kila aaminiye. Aliwaambia kwamba, ingawa walikuwa na huzuni kufuatia habari za kuondoka kwake, watafurahia tena kama vile mwanamke anavyokuwa na huzuni wakati wa kujifungua lakini kufurahia tena mtoto anapozaliwa.
Yesu alijua kwamba watabadilisha mawazo watakapoona utukufu wa Roho wake ndani yao na nguvu zilizokuwepo kwa kila mmoja wao kupitia kwa faida ya kutumia jina lake katika maombi. Alikuwa anawapa—na amewapa wote wamwaminio—“mamlaka yake,” haki ya kisheria ya kutumia jina lake. Jina lake linachukua mahali pake; jina lake linamwakilisha.
Tayari Yesu ashakuwa mtimilifu kwa ajili yetu. Alikwishampendeza Baba kwa ajili yetu; kwa hivyo, hakuna shinikizo juu yetu la kuhisi kwamba lazima tuwe na rekodi timilifu mwenendo mzuri kabla tuweze kuomba. Tukija mbele za Baba kwa jina la Yesu, tunaweza kukiri dhambi zetu, tupokee msamaha wake, na maombi yetu yajulikane naye.
Jina la Yesu linapotajwa na aaminiye kwa imani, mbingu yote husikiliza.