Una Nia Ya Kristo

Una Nia Ya Kristo

Maana, nani aliyeifahamu nia ya Bwana, amwelimishe? Lakini sisi tunayo nia ya Kristo. 1 WAKORINTHO 2:16

Katika Wakorintho 2:16, tunaambiwa tuna nia ya Kristo. Maelezo haya huwashangaza watu wengi. Iwapo haya hayangekuwa maneno ya Biblia, hawangeyaamini. Lakini Paulo hakuwa anasema hatuko wakamilifu au hatutawahi kukosea. Alikuwa anatuambia kwamba tunaweza kuwaza mawazo ya kiroho kwa sababu Yesu yuko hai ndani yetu. Shukuru kuwa si lazima tuwe na mawazo tuliyokuwa nayo wakati mmoja; tunaweza kuanza kuwaza anavyowaza.

Njia nyingine ya kutazama hili ni kurejelea ahadi ambayo Mungu alinena kupitia kwa Ezekieli: “Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama. Nami nitatia roho yangu ndani yenu” (Ezekieli 36:26–27).
Nia yako, moyo, na roho ni mpya ndani ya Kristo. Unakua kiroho na kuwa kama yeye kila siku—hicho ni kitu cha kushukuru kwacho!


Sala ya Shukrani

Asante, Baba, kwamba umenipa nia ya Yesu. Sihitajiki tena kuwaza mawazo ya kufadhaisha, yenye hofu na yasiyo na usalama. Kwa sababu ya Yesu, nia yangu imegeuzwa upya na ninaweza kuwaza mawazo chanya yaliyojaa imani kuhusu maisha yangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon