Unafikiria Nini Kujihusu?

Unafikiria Nini Kujihusu?

Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu. WAFILIPI 1:6

Ni muhimu kujitazama vile Maandiko yanavyosema juu yetu. Hakuna aliye mtimilifu; sisi wote tunaendelea kukua. Shukuru kuwa tunaweza kujua kuwa tunapendwa na kukubaliwa na Mungu tunapozidi kuwa watu anaotaka tuwe.

Mawazo haya yanaakisi picha yako binafsi inayotokana na Biblia ambayo unaweza kuwa nayo ndani ya Kristo:

  1. Ninajua Mungu ainiumba na ananipenda (tazama Zaburi 139:13–14; Yohana 3:16).
  2. Nina dosari na udhaifu, na ninataka kubadilika. Ninaamini Mungu anafanya kazi katika maisha yangu, kunibadilisha kidogo kidogo, siku baada ya nyingine (tazama 2 Wakorintho 3:18).
  3. Kila mmoja ana dosari, kwa hivyo mimi si mshindwa kwa sababu tu ya kukosa kuwa mtimilifu (tazama 2 Wakorintho 12:9).
  4. Hata nishindwe mara ngapi, sitakata tamaa, kwa sababu Mungu yuko nami kunitia nguvu na kunikimu (tazama Waebrania 13:5).
  5. Mimi binafsi si kitu, ilhali ndani ya Yesu mimi ni kila kitu ninachohitaji kuwa (tazama Yohana 15).
  6. Ninaweza vitu vyote ninavyohitaji kufanya—kila kitu ambacho Mungu ananiita nifanye kupita kwa Mwanawe Yesu Kristo (tazama Wafilipi 4:13).

Sala ya Shukrani

Baba, ninashukuru sana kwamba nina utambulisho mpya ndani yako. Haijalishi kile nimeambiwa au vile ninahisi siku yoyote ile, nitaamini Neno lako na kuamini kuwa kila kitu Neno lako linasema juu yangu ni ukweli.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon