Unahiari Kufundishwa?

Unahiari Kufundishwa?

Maana, ndugu zangu, angalieni mwito wenu, ya kwamba si wengi wenye hekima ya mwilini, si wengi wenye walioitwa bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu. —1 WAKORINTHO 1:26–27

Mtazamo wa haraka wa wanafunzi ambao Yesu alichagua unaonyesha kwamba Mungu wakati wote hachagui wale ambao wanaonekana kwamba wamehitimu. Haijalishi unahisi una upungufu wa vipawa, talanta au tajriba zipi—Mungu atakupa masomo na mafunzo yote unayohitaji kufanya kile alichokuitia kufanya.

Wakati wote sio kawaida, lakini Mungu atakutayarisha kwa njia yoyote ile atakayochagua. Wakati mwingine ya kiutaratibu, lakini mara nyingi sivyo. Mungu atatumia kila kitu katika maisha yako kukufunza iwapo unahiari kufunzwa. Ni jambo la huzuni kusema watu wengi wana miito mikuu juu ya maisha yao, lakini hawana uvumilivu wa kupitia matayarisho ambayo yanahitajika kuwaandaa kwa ajili ya kazi hiyo.

Esta alilazimika kuwa na mwaka wa maandalizi kabla ya kuruhusiwa kwenda mbele za mfalme. Kwa miezi kumi na miwili, alipitia kwa uvumilivu, utaratibu wa kusafishwa, na Mungu akamtumia kuokoa watu wake kutoka kwa njama ya uovu wa Hamani.

Iwapo unahisi kuwa hujahitimu vizuri kwa kitu ambacho Mungu anakuita ufanye, usiache hilo likukomeshe. Atakuwa mkufunzi wako. Jifunze anachokufunza msimu huu, na uwe tayari kuchukua hatua nafasi itakapotokea.


Mungu atakuandaa kwa ajili ya maono hayo.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon