Unapohisi Kukata Tamaa

Unapohisi Kukata Tamaa

Naamini ya kuwa nitauona wema wa Bwana katika nchi ya walio hai!—ZABURI 27:13

Kuna wakati ambao sisi wote tumsikitika. Litakuwa jambo la kushangaza iwapo tutapitia wiki nzima bila kukumbana na aina fulani ya masikitiko. Tunajitayarisha (kuelekezwa upande fulani) kitu kufanyika kwa njia fulani, na kisipofanyika tunavyotarajia, tunasikitika.

Masikitiko yasiyoshughulikiwa hugeuka na kuwa mtamauko. Tukibaki katika hali ya mtamauko au kukata tamaa kwa muda mrefu, tuna uwezekano wa kusawijika na kusawijika hutuacha bila uwezo wa kushughulikia lolote.

Wakristo wengi waliosawijika huishi maisha ya kushindwa kwa sababu hawajajifunza jinsi ya kukabiliana na masikitiko. Msawijiko wanaopitia mara nyingi ulianza na masikitiko madogo ambayo hayakushughulikiwa vizuri.

Sio mapenzi ya Mungu kwetu kuishi kwa masikitiko, kusawijika au kukandamizwa. Tunaposikitika, tunaweza kuchagua kukataa kusikitika ili tujiepushe na mtamauko, ambao utatusawijisha.

Tunapojifunza kuweka tumaini na uhakika wetu ndani ya Yesu (1 Wakorintho 10:4) na kumpinga shetani anaposhambulia (1 Petro 5:8-9), tunaweza kuishi katika furaha na amani ya Bwana, huru kutokana na mtamauko.


Chagua kumpinga shetani ili uweze kuishi katika ukamilifu wa maisha ambayo Mungu ametwaa kwa ajili yako kupitia kwa Mwanawe Yesu Kristo.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon