Unaweza kuvishinda vita leo

Unaweza kuvishinda vita leo

Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti; bali nia ya roho ni uzima na amani. Warumi 8:6

Hivi sasa, wewe na mimi tuko katikati ya vita. Ni mapambano ya kiroho, na tunapigana dhidi ya watawala wa giza la wakati huu, dhidi ya majeshi ya kiroho ya uovu (Waefeso 6:12). Tunahitaji kuwa na akili ya Roho Mtakatifu kushinda vita.

Cha kusikitisha, kuna waumini wengi wanaofanya kazi na akili ya mwili. Lakini kama tunataka kuishi kwa njia ambayo inaweza kubadilisha dunia yetu, basi tunapaswa kuacha kuishi katika mwili na kuanza kuishi katika Roho.

Kila mmoja wetu anahitaji kuendelea kufanya marekebisho ili kuweka tamaa zetu za kimwili chini kwa  udhibiti wa Roho Mtakatifu na tusiache hisia zetu au akili zetu zitudhibiti. Maandiko yanaelezea kwamba roho hupigana vita dhidi ya mwili na mwili hupigana vita dhidi ya roho, kwa hiyo huendelea kupingana kila mara. Ni vita!

Ibilisi anatuchukia, na anafanya kazi kwa muda mrefu, akijaribu kuhakikisha kwamba tunajipeana kwa mwili.

Wewe pekee, ndiwe unaamua nani anayefanikiwa katika maisha yako. Habari njema ni kwamba haufai kuwa chini ya mwili wako. Unaweza kuishi kwa Roho, na kuuleta mwili wako kulingana na mapenzi yake. Unaweza kushinda vita leo!

OMBI LA KUANZA SIKU

ungu, nataka kushinda vita leo. Ninataka kuwa na akili ya Roho Mtakatifu, ambayo ni maisha na amani. Ninachagua Roho wako leo. Nisaidie kuleta mwili wangu kulingana na mapenzi yako.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon