Unganishwa Naye

Unganishwa Naye

Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana… —YOHANA 15:5

Katika safari yetu ya Ukristo, mara nyingi huwa tunaishia kuwa na kanuni, utaratibu na mbinu, lakini bila uwezo wa kweli. Hilo ni ukweli haswa katika mafundisho ya imani, maombi, sifa, tafakuri, mafunzo ya Biblia, kukiri, vita vya kiroho, na kanuni zingine zote ambazo tumekuwa tukizisikia na kuzifanya. Yote ni mazuri, na tunahitaji kuyajua, lakini hayo peke yake hayawezi kutatua matatizo yetu.

Ni muhimu kukumbuka kwamba, hata kama mambo haya ni mazuri, ni njia tu za kupokea kutoka kwa Bwana. Hayatatusaidia hadi tujiunganishe na chanzo cha nguvu za kiungu.

Tunajiunganisha kupitia kwa uhusiano wa kibinafsi na Mungu, ambao huhitaji muda. Hatutawahi kuwa na ushindi wa kudumu katika maisha yetu wa Ukristo bila kutumia muda wetu binafsi katika mahali pa siri na kuwa na ushirika na Mungu. Ana mpango wako binafsi. Ukimwomba, atakuja ndani ya moyo wako na kuwa na ushirika nawe. Atakufundisha na kukuongoza katika njia unayofaa kufuata.

Jifunze kuitika kwa haraka vichocheo vya Roho Mtakatifu kwa uhusiano wa ndani na Mungu. Jitenge uwe naye katika mahali pa siri na utabarikiwa kwa wingi.


Ni katika uwepo wa Bwana tu ambapo huwa tunapokea nguvu za Bwana.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon