Uongozi wa Roho Mtakatifu

Uongozi wa Roho Mtakatifu

Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia. YOHANA 14:26

Roho Mtakatifu ndani yetu huwa kama polisi wanaodhibiti mwendo wa magari barabarani. Tukifanya vitu kwa njia sahihi, tunapata “kibali cha kuendelea” kutoka kwake, na tukifanya vitu kwa njia isiyo sahihi, tunapata “onyo la kutoendelea.” Ikiwa tuko karibu kujiingiza katika mashaka, lakini hatujafanya uamuzi kikamilifu kuendelea, tunapata “ishara ya onyo.”

Kadri tunavyosimama na kumwomba Mungu mwelekeo, ndivyo tunavyoathirika kwa ishara za Roho Mtakatifu zinazotoka ndani yetu. Shukuru kuwa hatupigii kelele wala kutusemesha kwa sauti ya juu, hunong’oneza tu kwa sauti ndogo ya utulivu (tazama 1 Wafalme 19:12) na kutujulisha kuwa tuko karibu kufanya makosa. Tunaposikiza na kutii kila mara, inakuwa rahisi kumsikiliza wakati mwingine. Atatuongoza kwenye upya wa maisha na amani ya ndani tukijiachilia kwake.


Sala ya Shukrani

Baba, nikiwa katika hali ambapo sina hakika iwapo nitaendelea au la, nisaidie kusikia sauti yako. Ninakushukuru kwamba una mwongozo ulio wazi kwa maisha yangu na kwamba utaniongoza na kunielekeza katika mpango wako juu ya maisha yangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon