Upendo Huwa Mgumu Wakati Mwingine

Upendo Huwa Mgumu Wakati Mwingine

. . . Wala sitamtolea Bwana , Mungu wangu sadaka za kuteketezwa nisizozigharimia. 2 SAMWELI 24:24 BIBLIA

Ikiwa Mungu anataka tusaidie watu, kwa nini hawezi kufanya ikawa rahisi na gharama ya chini? Acha nijibu swali hilo kwa swali lingine. Je, Yesu alijitoa kama dhabihu ili kununua uhuru wetu kutoka kwa dhambi na utumwa? Bila shaka alifanya hivyo. Alitoa kila kitu—na tunashukuru milele kwa wokovu wetu! Mojawapo ya njia ambazo tunaweza kuonyesha shukrani ni kwa kutoa ili kuwasaidia wengine.

Nimejifunza kwamba upaji wa kweli ni upaji ambao hutuathiri. Kupeana nguo zetu na vitu vya nyumba vilivyozeeka na kumalizia kwa tendo zuri, sio upaji wa kujitolea. Upaji wa kweli hufanyika tunapompa mtu kitu ambacho bado tunakihitaji, au kitu ambacho kitatugharimu.

Mungu alitupatia Mwanawe wa pekee kwa sababu anatupenda, kwa hivyo upendo utatusababisha kufanya nini? Usiache hali isiyofaa au dhabihu kukuzuia kupenda watu wengine kwa roho ya ukweli.


Sala ya Shukrani

Ninakushukuru, Baba, kwamba ulinipenda sana hata ukamtuma Mwanao, Yesu, ili afe kwa sababu ya dhambi zangu. Nisaidie kukumbuka kwamba upendo haujitumikii, lakini ni wa kujitolea na hautafuti mambo yake.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon