Kitu Kikuu Zaidi ya Hivi Vyote ni Upendo

Kitu Kikuu Zaidi ya Hivi Vyote ni Upendo

Takeni sana karama zilizo kuu. Hata hivyo nawaonyesha njia iliyo bora. 1 WAKORINTHO 12:31

Upendo unaingia katika nafasi gani kwenye orodha ya mambo yako muhimu? Yesu alisema, “Amri mpya nawapa, mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo” (Yohana 13:34 Biblia). Inaonekana kwangu kwamba Yesu alikuwa akisema upendo ndio kitu muhimu ambacho tunafaa kuzingatia. Mtume Paulo anaeleza kwamba “imani, tumaini, upendo…na katika hayo lililo kuu ni upendo” (1 Wakorintho 13:13).

Mojawapo ya vitu vingi vikubwa ambavyo tunafaa kumshukuria Mungu ni kwamba Mungu ni upendo. Kwa hivyo tukichagua kutembea katika upendo wake, tutakaa ndani yake. Ndiyo kwa sababu upendo ni kitu kikubwa sana ulimwenguni. Ndicho kitu kizuri cha kufanya katika maisha yetu na kukifanya vizuri zaidi.

Ninakuhimiza kujipa kibali cha kumwonyesha mtu upendo leo. Upendo haubariki tu watu wengine; hubariki pia anayependa.


Sala ya Shukrani

Baba, asante kwa kuwa unanipenda na unaonyesha upendo huo kila siku. Nisaidie kupokea upendo wako, na unisaidie kuwaonyesha wengine upendo huo.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon