Urembo wa Agano Jipya

Urembo wa Agano Jipya

Kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi. MATHAYO 26:28

Agano jipya ni kitu cha kushukuru kwacho milele. Ni agano lililo zuri zaidi na la juu zaidi kuliko lile la kale. Agano la kale lilianzishwa kwa damu ya wanyama, lakini jipya lilianzishwa kwa damu ya Yesu Kristo isiyo na dhambi. Chini ya Agano jipya, Yesu alitimiza au kuzingatia Sheria za agano la kale na kufa kwa ajili yetu ili kulipia dhambi na makosa yetu.

Yesu alichukua adhabu tuliyostahili na kuahidi kwamba iwapo tungemwamini pamoja na kuamini vitu vyote alivyotufanyia, angesimama mahali petu milele na wajibu wetu wa kuzingatia Sheria ungetimizwa ndani yake. Agano la kale lililenga kile binadamu angefanya, lakini agano jipya linalenga kile ambacho Mungu ametufanyia ndani ya Yesu Kristo (tazama Waebrania 8 na 9 kwa uchunguzi zaidi wa eneo hili)


Sala ya Shukrani

Ninakushukuru, Baba, kwa kuwa ninaweza kuishi katika nguvu za kazi ya agano jipya inayoweka huru. Asante kwa kuwa ulinipenda vya kutosha hata ukamtuma Yesu kufa kwa ajili ya dhambi zangu. Na asante kwamba ninaweza kuishi nawe katika uhusiano wa kibinafsi ulio wa ndani.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon