Usijidharau

Usijidharau

Mtu wa nia mbili husita-sita katika njia zake zote. YAKOBO 1:8 BIBLIA

Kujishuku hutufanya tuwe na nia mbili, na Yakobo 1:8 inafundisha kwamba mtu wa nia mbili hana uthabiti. Kwa kweli hawezi kusonga mbele hadi aamue kumwamini Mungu na kuamini mpango wa Mungu juu ya maisha yake.

Ninakuhimiza kuchukua hatua kubwa ya imani na uache kujishuku. Yaani, “usjidharau.” Una uwezo mwingi kuliko unavyofikiri. Unaweza kufanya mengi sana kuliko yale uliwahi kufanya zamani. Mungu atakusaidia iwapo utaweka imani yako ndani yake na uache kujishuku.

Kama kila mtu, utafanya makosa. Lakini, shukuru kuwa Mungu atakuruhusu kujifunza kutokana nayo na kwa kweli atafanya kazi nayo kwa mema yako iwapo utaamua kutoshidwa nayo. Shaka ikianza kutesa mawazo yako, anza kusema Neno la Mungu kutoka kinywani mwako—utashinda vita.


Sala ya Shukrani

Baba, ninashukuru sana kwamba unaweza kuchukua hata makosa yangu kuyageuza kuwa kitu kizuri. Ninaomba kwamba utanisaidia kuweka shaka kando na kukuamini kabisa. Asante kwamba ndani ya Kristo, nina kila kitu ninachohitaji; sihitaji kuwa na shaka tena.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon