Utakaso Huleta Nguvu

Utakaso Huleta Nguvu

Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi na tupige mbio kwa subira katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu. WAEBRANIA 12:1 BIBLIA

Ili kuishi katika ushindi, ni muhimu kuamua kuishi kwa ajili ya Mungu kwa vyovyote vile. Waebrania 12:1 inatuambia kuweka kando kila dhambi ituzingayo. Kimaadili, haiwezekani kuwa na mafanikio ya kiroho tukiwa na dhambi ya hiari inayojulikana katika maisha yetu. Simaanishi kwamba tuwe watimilifu kabisa ili Mungu atutumie, lakini ninasema kuwa lazima tuwe na nia yenye bidii kuhusu kuweka dhambi kando na maisha yetu.

Mungu anaposema kuna kitu kisicho sawa, basi hakiko sawa. Hatuhitaji kujadili, kunadharisha, kulaumu, au kuwa na visababu, au kujihurumia—tunahitaji kukubaliana na Mungu, kumshukuru kwa kutuonyesha, tuombe msamaha, na kufanya kazi na Roho Mtakatifu ili kuondoa milele chochote kisichofaa katika maisha yetu. Utakaso huleta nguvu, na kwa usaidizi wa Mungu, tunaweza kuishi maisha yenye vitu vingi na nguvu.


Sala ya Shukrani

Baba, ninashukuru kwamba huwa unanionyesha dhambi katika maisha yangu ili nikiuke dhambi hiyo na kuishi katika ushindi. Leo ninataka kuweka kando dhambi yoyote inizingayo na kuishi maisha matakatifu yenye utakaso kwa ajili yako. Asante kwa kuwa utanisaidia katika kila hatua njiani.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon