Utambuzi wa Haki yako

Utambuzi wa Haki yako

Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika yeye. —2 WAKORINTHO 5:21

Waaminio wanaoishi katika ushirika wa karibu na Mungu hawataweza kuwaza kuhusu jinsi walivyo wabaya. Watakuwa na mawazo yenye misingi yake katika haki ambayo huja kupitia kwa kutafakari kila mara kuhusu wao ni nani “ndani ya Yesu.”

Ilhali idadi kubwa ya Wakristo wanateseka kwa mawazo mabaya kuhusu vile walivyo wenye dhambi, au vile Mungu hapendezwi nao kwa sababu ya udhaifu na makosa yao. Ni wakati gani unaoharibiwa kwa kuishi chini ya hatia na hukumu?

Ninakuhimiza kufikiria kuhusu vile umefanywa mwenye haki wa Mungu ndani ya Yesu Kristo. Kumbuka: Mawazo hugeuka na kuwa matendo. Iwapo unataka kufurahia maisha ambayo Yesu alikufa kukupatia, ni muhimu kufungamanisha mawazo yako na Neno la Mungu.

Kila wakati wazo baya linalohukumu linapokuja katika nia yako, jikumbushe kwamba, Mungu anakupenda, na kwamba umefanywa mwenye haki ndani ya Yesu.


Unabadilika na kuwa bora wakati wote. Unakua kiroho kila siku. Mungu ana mpango mtukufu kwa ajili ya maisha yako.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon