Utu Mpya

Utu Mpya

Hata imekuwa mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya, ya kale yamepita tazama! 2 WAKORINTHO 5:17

Neno la Mungu hutufundisha kuwa tunapompokea Kristo Mwokozi wetu na Bwana, anatupatia utu mpya (tazama 2 Wakorintho 5:17). Anatupatia utu wake. Anatupatia pia Roho wa nidhamu na kiasi, ambaye ni muhimu katika kuturuhusu kuchagua njia za utu wetu mpya. Na anatupatia akili timamu (tazama 2 Timotheo 1:7). Hiyo ina maana tunaweza kufikiri kuhusu vitu kwa njia nzuri bila kutawaliwa na hisia.

Kila aaminiye anaweza kushukuru kwamba wakati mmoja tulikuwa wafu lakini sasa tuna vifaa vyote tunavyohitaji kwa maadili mapya kabisa. Kwa usaidizi wa Mungu tunaweza kuchagua Roho dhidi ya mwili na mema dhidi ya makosa. Roho zetu zilizofanywa upya sasa zinaweza kudhibiti nia na miili yetu au, kusema hilo kwa njia nyingine, mtu wa ndani anaweza kudhibiti mtu wa nje. Halafu tuweze kuishi ndani ya mpango wa Mungu juu ya maisha yetu.


Sala ya Shukrani

Baba, ninakushukuru kwamba mimi ni kiumbe kipya ndani yako. Ninafurahi sana kwa mwanzo mpya na utu mpya ambao umenipa. Nisaidie leo kuacha nyuma njia za zamani na kuishi maisha mapya ya furaha iliyotimilika na yenye ushindi ndani yako.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon