Vita Vya Nia

Vita vya Nia

Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. —Waefeso 6:12

Usomaji wa makini wa Waefeso 6 unatujulisha kwamba tuko vitani, na kwamba vita vyetu si vya wanadamu wenzetu lakini na mwovu. Adui yetu, Shetani, hujaribu kutushinda kwa uongo na ujanja, kupitia kwa mipango aliyopanga vizuri na hila ya kimaksudi.

Yesu alimwita shetani “baba wa uongo na vyote vidanganyifu” (Yohana 8:44). Hukudanganya wewe na mimi. Hutuambia vitu kutuhusu, watu wengine, na kuhusu hali ambavyo havina ukweli wowote. Mara nyingi huwa hatuambii uongo wote kwa wakati mmoja.

Huanza kwa kushambulia fikra zetu kwa kubuni ruwaza ya kijanja ya mawazo madogomadogo yanayokera, tuhuma, shaka, hofu, mishangao, fikra razini, na nadharia. Husonga taratibu na kwa tahadhari. Kumbuka ana mkakati kwa vita vyake Shetani ametusoma kwa muda mrefu na anajua tunachopenda na tusichopenda. Anajua kinachotukosesha usalama, udhaifu na hofu zetu. Anajua kinachotukera zaidi na huwa radhi kuwekeza kiasi chochote cha muda utakaopatikana kutushinda. Lakini tunaweza kumshinda adui kupitia kwa nguvu za Roho Mtakatifu na kupitia kujifunza ukweli wa Neno la Mungu!


Wewe ni zaidi ya mshindi kupitia kwa Kristo anayekupenda!

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon