Vitu Vyema Vyaja

Vitu Vyema Vyaja

Ndipo nikawaambieni, msifanye hofu, wala msiwache. Bwana, Mungu wenu, anayetangulia mbele yenu, ndiye atakayewapigania, kwa mfano wa yote aliyowafanyia huko Misri mbele ya macho yenu. —KUMBUKUMBU LA TORATI 1:29–30

Je, huwa unatazamia kila siku kwa moyo wa furaha na matarajio ya vitu vyema vinavyokuja, au huwa unaamka kila asubuhi katika hali ya kuogopa? Mtu anaweza kuogopa kwenda kazini, kuendesha katika msongamano wa magari, kusafisha nyumba au kukabiliana na watu wagumu. Woga ni aina ya hofu isiyotambulika ambayo shetani hutumia kuiba furaha yetu na kutuzuia kufurahia maisha. Hutuzuia kutembea katika mapenzi ya Mungu na kusonga mbele katika mipango ya Mungu ili kupokea baraka zake.

Woga hutufuata kwa nguvu na hauwezi kushindwa kwa utulivu. Kuruhusu hisia na mawazo hasi katika akili zako yataiba furaha na amani yako. Lakini unaweza kumwamini Mungu kukusaidia na chochote unachohitaji. Na anapokupa neema, kitu ulichokuwa ukiogopa kitaonekana kuwa si kibaya hata hivyo. Tunaweza kuchagua kuamini kwamba Yesu hututangulia na kututengenezea njia. Mradi unapoonekana kuwa mgumu au usiopendeza, usianze kuuogopa. Iwapo utaufanya, hata hivyo huenda utaufurahia!

Kama Wakristo, tunaweza kupata furaha hata katika hali mbalimbali kwa sababu uwepo wa Mungu uko nasi. Tunaweza tukafurahia maisha yetu naye katikati ya hali ngumu na yenye taabu. Furaha yetu inatoka kwa yule aliye ndani yetu, si kwa kile kilichotuzunguka.

Tukilenga mawazo yetu kwacho, tunaweza kufurahia kila tunalofanya maishani. Mungu anapokuongoza, anakukimu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon